Utatu Mtakatifu Mfano wa Umoja

Utatu Mtakatifu Mfano wa Umoja wa Kifamilia

Sherehe ya Utatu Mtakatifu

 

Waheshimiwa Wanafamilia ya Mungu,

Leo tunaadhimisha fumbo kubwa sana katika imani yetu, FUMBO LA UTATU MTAKATIFU. Tunaadhimisha fumbo la imani yetu kuwa MUNGU NI MMOJA KATIKA NAFSI TATU, MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU. Tumwombe Mungu azibariki familia zetu ili tuwe na umoja kama wao walivyo na umoja katika familia ya mbinguni.

Nami nawakaribisha tutafakari juu ya mambo mawili

 1. Ukweli kuhusu Utatu Mtakatifu
 2. Mfano wa Utatu Mtakatifu katika kuishi Umoja wa Kifamilia

 UKWELI KUHUSU UTATU MTAKATIFU

 • Kuelewa muungano na umoja uliopo katika nafsi hizi tatu katika umungu mmoja si jambo rahisi kwa akili zetu za kibindamu.

 

 • Lakini leo ningependa kuchukua msimamo wa Mt. Augustino aliyesema kuwa mafumbo kama haya katika imani yetu ni kama mifupa katika nyama.

 

 • Kama tusivyoitupilia mbali mifupa moja kwa moja na nyama iliyo juu yake bali tunakwangua nyama yote na kuachana na mifupa, na haya mafumbo hatuwezi kuyakimbia moja kwa moja tutafanya tuwezalo ili kuelewa kinachoweza kueleweka; ikibaki mifupa kabisa tutaacha.

 

 1. Namna ya kuuelewa Utatu Mtakatifu

 

Tutofautishe Ukweli wa Kisayansi na Ukweli wa Ufunuo

 • Wale wasioamini katika Utatu Mtakatifu, hutulamu Wakatoliki kuwa tunaabudu miungu wengi-miungu watatu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

 

 • Wanahoji kuwa katika mahesabu 1+1+1 = 3, sasa kwa nini sisi tuseme Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu ni Mungu Mmoja?

 • Katika hoja hiyo tatizo linalojitokeza ni kuchanganya namna mbili za maarifa au ukweli. Kuna maarifa au ukweli wa Kisayansi unaojulikana kwa majaribio na utafiti (Scientific or Empirical Truth).

 • Kuna maarifa au ukweli wa Ufunuo (Revealed Truth) unaopatika si kwa kanuni za kisayansi bali kwa kufunuliwa. Ukweli wa 1+1+1 = 3 ni ukweli wa kisayansi. Ukweli wa Mungu Mmoja katika Nafsi Tatu ni ukweli wa ufunuo ambao hauwezi kujaribiwa kwa kanuni za kisayansi kama kujumlisha.

 • Lakini tatizo jingine lililomo katika hoja yao hiyo ya kujumlisha ni kwamba kwa nini wajumlishe? Kwani hawawezi kuzidisha ikawa 1x1x1 = 1?

Mtakatifu Paulo anakubaliana na namna hizo mbili za maarifa akisema

 “Basi, sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho. Mtu wa kidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo mambo hayo ni upumbavu mtumpu; yanapita akili yake; maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaada wa Roho. Maandiko yasema, ‘Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Lakini sisi tunayo akili ya Kristo. (1Kor.2:13-16).

 1. Mifano ya Ukweli wa Kisayansi na Ukweli wa Ufunuo

  1. Kwamba kulikuwa na mwanamke anaitwa Maria ni ukweli wa kisayansi. Historia inaonyesha hivyo. Lakini kwamba huyu Maria alimzaa Mungu na alikuwa bikira kabla ya kuzaa, wakati anazaa na baada ya kuzaa, huu ni ukweli wa ufunuo.

 2. Kwamba palikuwa na mwanaume anaita Yesu ni ukweli wa kisayansi. Historia inadhihirisha hayo. Lakini kwamba huyu Yesu alikuwa Mungu ni ukweli wa ufunuo.

 3. Hata wanafalsafa wamejitahidi kutumia akili yao kuonyesha (to prove) kwamba lazima Mungu yupo. Lakini hata wao wamemfahamu Mungu kama Nguvu inayosukuma na kuongoza vitu vyote ulimwengu (God as an uncaused cause, unmoved Mover). Hawakuweza kumjua Mungu kama sisi tumjuavyo kwamba ni Mungu mwenye upendo, msamaha na anayetufariji katika shida zetu. Haya tumeyafahamu si kwa kutumia akili za kibinadamu tu bali kwa ufunuo.

 • Ukweli wa Kimungu unafunuliwa na Roho wa Mungu na wenye Imani tu waweza kuelewa.

 • Bwana Yesu ametwambia

Huyo Roho wa ukweli atawaongoza katika kweli yote” (Somo la II)

Kwa hiyo

 • Si vizuri kuingia katika mabishano na watu wa namna hiyo maana mtakuwa mkiongea katika frequency tofauti kama Yesu na Nikodemo.

 • Si vizuri kubishana sana au kupinga mafundisho ya Kanisa au ukweli wa Biblia. Ukikutana na lolote ambalo hulielewi ama katika Biblia au katika mafundisho ya Kanisa usiseme ‘mambo ya wakatoliki hayaeleweki’ bali useme ‘akili zangu ni ndogo kuelewa ukweli huu.’ Fanya juhudi kuelewa utakavyoweza.

 • Yatakayokushinda “Inamisha kichwa mpaka nchi na useme NASADIKI.

 

 1. Ufunuo juu ya Utatu Mtakatifu katika Biblia

 

 • Kama Bwana Yesu ametwambia

Huyo Roho wa ukweli atawaongoza katika kweli yote” (Somo la II)

 

 • Kuna ukweli unaohitaji kufunuliwa na Roho Mtakatifu ili kuuelewa. Mojawapo ya ukweli huo ni juu ya Utatu Mtakatifu.

 

 • Mungu ndiye aliyejifunua hivyo kwamba ni Mungu mmoja katika nafsi Tatu. Ufunuo huu unapatikana katika biblia na katika mapokeo ya Kanisa.

 • Leo, naomba tuangaliye ni sehemu gani za Biblia zinazotufunulia ukweli huu kuwa Mungu ni Mmoja katika Nafsi Tatu.

 

 

 1. Mwa 1:1-2Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu akatulia juu ya uso wa Maji.”

 1. Meth 8: 1-36 Hekima (ambaye ni Kristu) anasema “Kabla Mungu hajaumba dunia na mashamba yake, nilikuwa pamoja naye kama fundi stadi” (Somo la I)

Katika historia ya wokovu wetu tumemjua Mungu Baba kama Muumbaji, Mungu Mwana kama Mwokozi na Mungu Roho Mtakatifu kama Mfariji. Lakini sehemu hizo mbili za Biblia zinaonyesha kuwa katika hayo yote Nafsi zote Tatu za Utatu Mtakatifu zilishiriki.

 1. Mwa 1:24 “Mungu akasema ‘Natumfanye mtu kwa mfano wa sura yetu.” Mungu akasema (mmoja) …kwa sura na mfano wetu (wingi)’”. Hii tayari inatuonyesha kuwa Mungu ni Mmoja katika Nafsi zaidi ya moja.

 1. 6: 4 Sikiliza ee Israel Bwana Mungu wetu Bwana ndiye Mmoja.”

 1. Mwa 18:1-15Mungu alimtokea Abraham penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake,…akaona watu watatu wamesimama

 1. Jn 14: 15-17 Mkinipenda mtazishika amri zangu. Nami (Mwana) nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine…ndiye Roho wa Ukweli.”

 

Kwa hiyo, hiki ndicho chanzo na msingi wa imani yetu kuwa Mungu ni Mmoja katika Nafsi Tatu.

Tuna uhakika na ufunuo huu na ukweli huu kwa sababu aliyetufunilia ni Mungu mwenyewe Yesu Kristu aliye nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu.

 

TUJIFUNZE NINI KUTOKA UTATU MTAKATIFU?

  1. Tuwe wamoja kama Utatu ulivyo na Umoja
 • Katika Utatu huu kuna umoja wa ajabu na mshikamano wa ajabu na ushirikiano usio wa kawaida. Huu umoja ndio unapaswa kuwa msingi na mfano wa kuigwa katika umoja tunaopaswa kuuonyesha katika mahusiano yetu, katika familia zetu, katika jumuiya zetu na katika nchi yetu.

 • Katika kuanzisha Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristu Kanisa Katoliki lilichota katika Umoja uliopo katika Utatu wa Kimungu pia na Umoja unaodhihirishwa na Jumuiya ya Wakristu wa kwanza.

 

 

 

Kristu aliomba

 

Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.” (Jn 17:21).

2. Tuwe na Ushirikiano

 • Ni kweli tumefunuliwa na kumjua Baba kama Muumbaji, Mwana kama Mkombozi na Roho Mtakatifu kama Mfariji.

 

 • Lakini katika yote haya hawakuachana. Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu walikuwepo na kushiriki katika uumbaji.

 

 • Katika kitabu cha mwanzo tunasoma …na Roho wa Mungu ikatulia juu ya uso wa Maji”(Mwa 1:2).

 • Aidha, Yohana anatwambia hivi

 

Hapo mwanzo kulikuwa Neno naye Neno alikuwa kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika(Yoh.1).

 

 • Katika kutukomboa Mungu Baba na Mungu Roho hawakumwachia Mungu Mwana ahangaike peke yake. Wote walikuwepo kama Yohane anavyotwambia

Yesu akajibu, ‘wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo ninyi nyote mtatawanywa kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yangu yu pamoja nami’”(Yn.16:32).

 

 • Luka anatwambia tena kuwa Yesu alipokuwa Gethseman alilia akasema

Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki… hapo, malaika kutoka mbinguni akamtokea ili kumtia moyo(Lk.22:42-43).

 

 • Basi tuwe na Umoja kama Utatu Mtakatifu ulivyo na Umoja.

 

 • Tuondoe lugha ya shauri yako, umeyataka mwenyewe; utajiju.
 • Baba, Mama na Watoto tuwe na mawasiliano mazuri na kusaidiana katika kutafuta na katika kushiriki matunda ya kazi yetu.

 • Yanapokuja magumu kwa mmoja wetu tushirikiane kuyatatua. Tulie na wanaolia na kufurahi na wanaofurahi.

 • Mtoto akipata shida katika masomo yake tusimuache kuhangaika peke yake. Tuwe naye katika kufanikiwa na katika shida.

 • Tuzingatie tena wosia wa Paulo

Hatimaye ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. Salimianeni kwa busu takatifu(2Kor 13:11-14).

Comments are closed.

Quote of the Week
Quote of the Week

"Je, Wanipenda?"

November 2019
M T W T F S S
« Oct    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
Find me on Facebook
Follow me on twiter